Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu ya ndimu, limau katika kuongeza damu mwilini

58077 Pic+ndimu

Fri, 17 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hivi unajua ndimu na limao huongeza damu mwilini mwilini?

Wakati wataalamu wa masuala ya lishe wakisisitiza ulaji wa vyakula tofauti ili kuupa mwili virutubisho vyote muhimu, kila tunda lina mchango mkubwa mwilini mwaka.

Kama ulikuwa hujui, basi ungana nami katika makala hii ili kufahamu kwa undani jinsi limao na ndimu zilivyo na vichocheo vya kuongeza damu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na dhana potofu kwa jamii juu ya faida na matumizi ya ndimu na limau na faida zake mwilini mwa binadamu.

Si ajabu kusikia mtu akisema matumizi ya ndimu na limau si mazuri kwa sababu yanasababisha upungufu wa damu jambo ambalo si kweli hata kidogo.

Mtaalamu wa lishe kutoka kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Elizabeth Lyimo anasema jamii inapaswa kufahamu kuwa ndimu na limau ni matunda yenye vitamini C ambayo husaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma.

Pia Soma

Anasema madini ya chuma ni muhimu katika kutengeneza chembechembe nyekundu za damu.

“Kwa mantiki hiyo matumizi ya ndimu na limau ni kichocheo kimajawapo cha kuongeza damu mwilini na wala si kupunguza kama watu wanavyodhani,” anasema Elizabeth.

Elizabeth anaasa ifahamike kwamba ndimu na limao husaidia kuongeza hamu ya kula hasa kwa mtu anayepata kichefuchefu na kutapika hivyo ulaji wa mara kwa mara wa matunda haya unakusaidia kukupa kichocheo ambacho kitasiaida kuongeza damu mwilini.

Mtaalamu huyo anasisitiza kuwa ni muhimu kuzingatia ulaji wa vyakula mchanganyiko ili kupata virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwani hakuna chakula kimoja kinachotosheleza mahitaji yote ya mwili.

Chanzo: mwananchi.co.tz