Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu! Daktari aliyemtoa mtoto tumboni kisha kumrudisha

Oluyinka Olutoye.jpeg Dk. Oluyinka Olutoye (kulia)

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inawezekana umesikia mengi katika ulimwengu huu ya kushangaza, kufurahisha na mengine ya kuhuzunisha sasa basi nakuongezea na hili la leo, kutana na Daktari mwenye asili ya Nigeria, Dk. Oluyinka Olutoye alipata mafanikio makubwa ya upasuaji alipomfanyia upasuaji mtoto aliyekuwa tumboni.

Lynlee Boemer ni mtoto wa kike ambaye alipitia safari isiyo ya kawaida, alikabili hali ya kutishia maisha yake kabla ya kuzaliwa kwake.

Wakati mama yake, Margaret, alipokuwa na mimba mwaka wa 2015, alipata uvimbe unaojulikana kwa jina la teratoma sacrococcĂ­geo uligunduliwa ukikua kwenye uti wa mgongo wa Lynlee akiwa ndani ya tumbo la mama yake.

Dk. Oluyinka katika Hospitali ya Watoto ya Texas alimtoa Lynlee kutoka tumboni mwa mama yake akiwa na wiki 23, wakamfanyia upasuaji maridadi kuondoa sehemu kubwa ya uvimbe huo, kisha wakamrudisha kwenye uterasi.

Baada ya kukabiliana na hali hiyo mbaya, Lynlee alizaliwa akiwa na wiki 36 na siku 5, akafanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa uvimbe, na sasa yeye ni mtoto mchangamfu na mwenye furaha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live