Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maabara za EAC zafanya vipimo 600,000 vya Corona

Mobil Pic Maabara za EAC zafanya vipimo 600,000 vya Corona

Tue, 26 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani vipimo 600,000 vya Corona vimefanyika chini ya mradi wa Awamu ya Kwanza wa Maabara zinazohamishika unaoratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Hayo yamebainishwa wakati wa mkutano wa mtandao wa kikanda wa maabara za kumbukumbu za afya ya umma kwa magonjwa ya kuambukiza.

Maabara hizo zimefanya kazi kubwa kwa kuhamasisha nchi wanachama katika kupambana na janga hilo.

"Maabara hizi zimefanya vipimo zaidi ya 600,000 vya Corona kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki" imesema taarifa ya EAC.

Mkutano huo, ulisisitiza kuwepo kwa mpango kabambe wa kuunganisha mradi huo katika maabara za kitaifa za afya ya umma na wizara za afya zilizopo katika mataifa ya EAC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live