Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maabara ya Sh6 bilioni kujengwa KCMC

MAABARAAA Maabara ya Sh6 bilioni kujengwa KCMC

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitaliya rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) imepanga kuanza kwa safari ya utalii wa kitabibu baada ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo kuzindua rasmi eneo litakapojengwa maabara ya kisasa itakayogharimu zaidi ya Sh6 billion.

 Akizungumza katika uzinduzi huo leo Julai 8, 2022, Askofu Shoo amesema hiyo ni hatua kubwa kwa Afrika Mashariki na kati, kwani itasaidia kuboresha huduma ya afya hasa katika kufanya utambuzi wa viini vya magonjwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi, amesema kuwa maabara hiyo itakua ni kituo cha umahiri cha kitabibu ambacho kimelenga kuboresha upimaji wa magonjwa,

“Tunategemea kufanya vipimo vyo hali ya juu ambavyo hapo awali havikuwezekana. Wagonjwa walisafiri na kwenda kufanya vipimo hivyo nje ya nchi, hivyo tunategemea kutoa huduma yenye ubora hasa ukizingatia waziri wa Afya, Ummy Mwalimu anisimamia ubora wa huduma hii,” amesema Makubi.

Awali akielezea mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji hospitali hiyo, Gileard Masenga amesema wamemejikita katika mihimili mitatu, ambayo ni tiba, tafiti na mafunzo, hivyo ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa utachagiza utoaji huduma bora kutoka kwa wabobezi.

“Hospitali yetu inatoa huduma bobezi, hivyo maabara hii itasaidia kupatikana kwa huduma bora yenye uhakika na ndani ya muda mfupi”

Ameongeza kuwa zaidi ya Sh6 bilioni zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa maabara hiyo huku ujenzi ukichukua miezi 12 hadi 16, ambapo ujenzi huo utafanyika ndani ya awamu mbili.

Naye Balozi wa Ujerumani nchini, Regina Hess amesema ujenzi wa maabara hiyo wanaoufadhili umelenga kuboresha huduma za afya nchin

Chanzo: www.tanzaniaweb.live