Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KUHARAKISHWA

338d6328e342044ff5e082ae81553c27.jpeg MUSWADA WA BIMA YA AFYA KWA WOTE KUHARAKISHWA

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto imesema ipo kwenye hatua za mwisho kuandaa Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote na kuuwasilisha bungeni Juni mwaka huu badala ya Septemba kama ilivyokuwa

imepangwa awali.

Waziri wa wizara hiyo, Dk Doroth Gwajima alisema hayo bungeni jijini Dodoma jana, wakati akichangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Alisema wizara hiyo imeupokea mchakato wa kuandaa muswada huo na unafanyiwa kazi usiku na mchana kuhakikisha unawasilishwa bungeni katika

mkutano unaoendelea.

Alisema pia wizara hiyo katika kipindi hiki itajikita katika kudhibiti magonjwa na kutibu.

Kuhusu uhaba wa vifaa, Dk Gwajima alisema wizara hiyo imeomba Sh bilioni 64 za kununua vifaa tiba na vitendanishi.

Alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha, wizara hiyo inakusudia kuomba

Bunge liidhinishe Sh bilioni 219 kwa ajili ya manunuzi kuongeza huduma za kibingwa hadi katika hospitali na vituo vya afya.

Dk Gwajima alisema kutokana na kuboresha huduma za kibingwa, rufaa za watu kwenda kutibiwa nje ya nchi zimepungua kutoka 164 kwa mwaka 2015/16 hadi rufaa mbili 2019/2020. Wizara hiyo pia imetenga Sh bilioni 144.9

kwa ajili ya kuajiri watumishi ambao watakwenda kufanya kazi katika vituo vya afya 487 vilivyojengwa kwenye halmashauri kwa lengo la kusogeza huduma hizo katika hospitali mbalimbali zikiwemo 102 zilizojengwa katika halmashauri.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Ummy Mwalimu alisema

bado kuna uhaba wa zahanati, vituo vya afya na hospitali, hivyo wizara hiyo itakamilisha ujenzi wa vituo 52 na hospitali 68 katika halmashauri ambazo hazina hospitali.

Pia alisema Rais Samia Suluhu Hassani ametoa agizo na kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga hospitali 24 katika halmashauri ambazo hazina hospitali hizo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz