Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MUHAS yaiangukia Serikali ujenzi kituo cha ubobevu Mloganzila

Moyo Mloganzila.jpeg MUHAS yaiangukia serikali ujenzi kituo cha ubobevu Mloganzila

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi Muhimbili (Muhas) umeiomba Serikali kuanzisha kituo cha matibabu ya magonjwa ya moyo Mloganzila ili kukiwezesha kituo kipya cha mafunzo ya ubobevu kukamilika.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Desemba 6, 2021 na Makamu Mkuu wa Chuo cha Muhas, Profesa Andrea Pembe wakati wa ufunguzi wa kituo cha umahiri cha Afrika Mashariki cha Chuo Kikuu kishiriki cha magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

“Kuanzisha kituo hiki cha mafunzo ya ubobevu pasipo uwepo wa hospitali ya magonjwa ya moyo eneo hili bila hivyo kituo hiki kitakua hakijakamilika,” amesema Profesa Pembe.

Mwenyekiti wa baraza la Muhas, Dk Harrison Mwakyembe amesema lazima kuwe na awamu ya pili ya mradi ili kukamilisha kituo cha matibabu.

“Bila kuwa na sehemu ya mafunzo kwa vitendo bado kituo hiki kitakua hakijakamilika, tunaomba iwepo awamu ya pili ya mradi huu. Katika awamu ya pili kutakuwa na kituo cha matibabu cha magonjwa ya moyo chenye vitanda 300,” amesema Dk Mwakyembe.

Amesema Tanzania ilichukua nafasi ya kujenga kituo hicho wakati Kenya ikijenga kituo cha mafunzo ya ubobevu wa magonjwa ya figo.

“Uganda wao wanajenga kituo cha ubobevu wa magonjwa ya saratani, Rwanda kituo cha uhandisi na tehama na Burundi wanajenga kituo cha mafunzo ya sayansi ya Lishe,” amesema Dk Mwakyembe.

Mradi huo uliojengwa kwa udhamini wa benki ya maendeleo ya Afrika kwa kutoa mkopo wa riba nafuu kiasi cha Sh21.6 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live