Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSD yakamilisha ujenzi wa viwanda vya dawa 7 ndani ya siku 365

Msd Boss.jpeg Mkurugenzi Mkuu wa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Mhidze

Thu, 30 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BOHARI ya Dawa (MSD) imefanikiwa kujenga viwanda saba vya kuzalisha dawa zikiwamo za vidonge, mipira ya mikono (cloves) vitakasa mikono, barakakoa na dawa za watoto ndani ya mwaka mmoja.

Aidha, inatarajia kuanzisha kiwanda kingine cha dawa za ngozi, yakiwamo mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi na dawa za meno.

Mkurugenzi Mkuu wa (MSD) Meja Jenerali Gabriel Mhidze, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wa bohari hiyo, mafanikio na mipango mikakati ya baadae.

Amesema tangu ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mei, mwaka jana, kwa kushirikiana na wataalam wake, waliandaa maandiko ya kuanzisha viwanda hivyo kwa lengo la kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini.

"Tumeanzisha viwanda saba kwa gharama ya Sh. bilioni 16 tu, wakati kwa kawaida kiwanda kimoja kinajengwa kwa Sh. bilioni 40. Tutaendelea kujenga vingine kikiwamo cha kuzalisha dawa za ngozi ikiwamo mafuta ya watu wenye ualibino," amesema.

Amesema kiwanda hicho, ambacho mashine zake zimeshafika kitazalisha pia dawa za meno na dawa za macho.

Mkurugenzi Mkuu huyo ameeleza zaidi kuwa, kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono (cloves) kilichopo Idofi, Makambako mkoani Njombe, kinatarajiwa kuanza uuzalishaji Novemba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live