Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSD yafikia asilimia 95 usambazaji dawa Kyela Mbeya

Dawa MSD yafikia asilimia 95 usambazaji dawa Kyela Mbeya

Fri, 21 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bohari ya Dawa (MSD) imefikia asilimia 95 ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba Wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Hatua hiyo imefikiwa mbali ya changamoto zilziopo ikiwemo katika kijiji cha Ikombe ambacho kinazungukwa na Ziwa Nyassa hivyo, kukosa barabara na ziwa linapochafuka dawa na watumishi kuwa hatarini.

Akizungumza jana wilayani humo Mfamasia wa Wilaya ya Kyela Emanuel Chacha amesema hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya wilayani Kyela mkoani Mbeya ni asilimia 95.

Alisema, hatua hiyo inafikiwa mbali na changamoto zilizopo katika kijiji cha Ikombe kilichopo kisiwani mwa Ziwa Nyasa.

“Tuna vituo 37 vinavyopata dawa na vifaa tiba kwa mfumo wa kielektroniki wa ELMIS kati ya vituo hivyo vyote vinafikika kasoro kimoja ambacho kipo kisiwani katika kijiji cha Ikombe kilichozungukwa na Ziwa Nyasa.

“Kutokana na juhudi za serikali kituo hicho pia kinapokea vifaa vya afya kwa asilimia 90 kutoka MSD,”alisema.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwa sekta ya afya nchini.

Alisema, hatua hiyo ni matokeo ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora na kwa wakati na kuboresha huduma kwa wananchi.

Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ikombe Dk.Joshua Katabazi, alisema ufikishaji wa dawa katika zahanati hiyo umekuwa na changamoto kutokana na kukosekana kwa barabara na kijiji kuzungukwa na Ziwa Nyasa.

Alisema,kituo hicho kinatumia njia ya majini na kinapokea dawa na vifaa tiba kila mwezi kutoka MSD hivyo upatikanaji wa vifaa vya afya kuwa wa asilimia 90.

“Kunachangamoto ya usafirishaji wa dawa kutoka Matema hadi hapa lakini serikali yetu inahakikisha maboresho sekta ya afya wanakijiji wa Ikombe wanakuwa wanufaika na sisi watoa huduma tunajivunia wananchi kupata dawa, vipimo na matibabu yote wanapofika kituoni,”alisema.

Kwa niaba ya wananchi wa Ikombe Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Ezekiel Mwamgunda, alisema wanaishukuru serikali mbali ya kuwapo kwa changamoto ya kupitisha dawa katika maji zimekuwa zikifika kwa wakati.

“ Kuna muda Ziwa linachafuka hivyo kuwa na hatari ya dawa na watumishi wa MSD kuzama ombi langu kwa serikali kuona haja ya kujenga barabara, mazingira haya ni hatarishi na hali inapokuwa mbaya zaidi inabidi wananchi wajitolee kupita pori kwa pori kufuata dawa kule ng’ambo eneo la Matema,”alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live