Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSD mbioni kusaini mkataba usambazaji dawa Sadc

82171 Sadc+pic MSD mbioni kusaini mkataba usambazaji dawa Sadc

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Bohari Kuu ya Dawa nchini Tanzania (MSD) ipo katika mchakato  wa kusaini mkataba na nchi 15 za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kuanza kusambaza dawa.

Hilo litakwenda sambamba na kutoa mafunzo kwa watendaji kutoka nchi wanachama kuhusu namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa uagizaji dawa unaotumiwa na MSD.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Oktoba 29, 2019 meneja manunuzi ya pamoja ya nchi za Sadc wa bohari hiyo, Marco Masala amesema kuna mifumo mingi imeundwa kushughulikia manunuzi hayo na tayari MSD ina kitengo maalum kwa ajili ya kazi hiyo.

“Tulitangaza tenda Aprili, 2019 baada ya kufanya kikao cha pamoja cha kuandaa miongozo na mfumo wa mnyororo wa ugavi Machi, 2019.”

“Mchakato ulikuwa mrefu na sasa tupo kwenye hatua ya kusaini mkataba, kilichobaki ni kuutumia mkutano huu (wa mawaziri wa afya nchi za Sadc)  wawahamasishe watendaji waanze kuleta oda,” amesema Masala.

Amesema MSD imeandaa mfumo wa Tehama utakaosaidia  mnyororo huo, “mfumo huu utasaidia kuanzia uagizaji, uzalishwaji kila kitu. Mfumo unaona mpaka utakavyomfikia mtumiaji katika nchi husika na tutaandaa mafunzo namna ya kutumia mfumo wa manunuzi ya dawa.”

Pia Soma

Advertisement
Masala amesema changamoto zilizochelewesha mchakato huo ni kuchelewa kuwa na mfumo wa pamoja wa kudhibiti ubora.

“Hili ni miongoni mwa mambo tutakayoyazungumzia katika mkutano ujao, kuna changamoto za uchache wa viwanda katika nchi za Sadc na hata tulivyonavyo bado vina changamoto kubwa katika uzalishaji,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz