Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MSD kuboresha upatikanaji wa Dawa Zanzibar

Msd Znz MSD kuboresha upatikanaji wa Dawa Zanzibar

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya ya Zanzibar imetiliana saini Mkataba wa Makubaliano na Bohari ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya, hasa dawa visiwani humo.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Amour Suleiman Mohamed, amesema mkataba huo ni muendelezo wa makubaliano ya muda mrefu kati ya Bohari ya Dawa Zanzibar (CMS) na MSD kuimarisha upatikanaji wa huduma za dawa zenye ubora zaidi, nchini Tanzania.

Makubaliano hayo yamehusisha masula mazima ya utaalamu wa kuwajengea uwezo watumishi, kuimarisha miundombinu ya Bohari ya Dawa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara, uhifadhi wa dawa na vifaa tiba pamoja na matumizi ya TEHAMA.

Aidha ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imeweka vipaumbele vya kuimarisha huduma za afya ikiwemo masula ya dawa kama ilivyoanishwa katika mkataba huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live