Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI yatoa tamko mgonjwa aliye-kiss na mpenzi wake wodini

IMG 20230711 WA0001 MOI yatoa tamko mgonjwa aliye-kiss na mpenzi wake wodini

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetoa ufafanuzi kuhusu uvunifu wa maadili ulivofanywa na Mgonjwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa Mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023 ambapo katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na Mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba Mpenzi wa Mgonjwa huyo si Mtumishi wa Taasisi ya MOl, aidha tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia Wahusika kuendelea na kitendo hicho a Menejiment inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa Wahusika”

“Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna Mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video, Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na Mgonjwa huyo pamoja na Mpenzi wake, vilevuls Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na Mgonjwa jirani”

“Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unaozuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini, Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa Wagonjwa wakati Ndugu wanawatembelea Wagonjwa wodini.” ——— MOI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live