Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI yapokea wagonjwa watatu wa kiharusi kila siku

Mooi Pic Data MOI yapokea wagonjwa watatu wa kiharusi kila siku

Tue, 20 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesema kila siku inapokea wagonjwa watatu wenye tatizo la kiharusi (stroke).

Hayo yameelezwa leo Septemba 20 na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Laurent Mchome katika kambi maalumu ya upasuaji wagonjwa 12 wenye matatizo ya uvimbe kwenye ubongo na matatizo yanayohusu utu wa mgongo.

Kambi hiyo ya siku tatu ni ushirikiano baina ya MOI na Hospitali ya Ramaiyah Medical Collage Memorial ya Bangalore ya nchini India.

Dk Mchome amesema tatizo la kiharusi limekuwepo kwa muda mrefu na wanaendelea kutafuta teknolojia zaidi ya kuutibu ugonjwa huo.

"Zipo aina nyingi za kiharusi lakini wagonjwa wengi tunapwapata ni wale ambao damu imevilia kwenye ubongo, tatizo hili ni kubwa sana, kwenye maabara yetu tunawafanyia uchunguzi tukiona wanahitaji upasuaji ndipo tunawafanyia upasuaji," amesema.

Amesema miaka ya nyuma wagonjwa hao walikuwa wakipatiwa huduma saidizi na wakipata nafuu hupelekwa nje ya nchi kutibiwa akini sasa wanatibiwa hapa nchini.

Advertisement Chanzo kikubwa cha tatizo hilo Dk Mchome amesema ni shinikizo la juu la damu.

"Wagonjwa wengi wenye shinikizo la juu la damu ambao hawatumii dawa kwa kufuata mpangilio maalumu walioelekezwa na wataalamu wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu, pia wapo wanaopata lehemu kwe damu wapo kwenye hatari ya kupata vivimbe ambavyo hupasuka na mtu kupata kiharusi," amesema.

Akizungumzia kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respecious Boniface amesema, kambi hiyo maalumu ilianza Septemba 19 na itahitimishwa Septemba 21.

"Tunategemea wagonjwa 12 watafanyiwa upasuaji mkubwa wa kibobezi, kati ya hao saba watafanyiwa uchunguzi wa tiba kichwani bila kufungua fuvu, watano ambapo kati ya hao 12 wapo watakaofanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo kupitia tundu dogo," amesema.

Chanzo: Mwananchi