Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI yafanya upasuji bila kufungua fuvu kwa watu 120

285899f3d2635b6b22f091a16147bb31 MOI yafanya upasuji bila kufungua fuvu kwa watu 120

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dk Respisious Boniface amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu, zaidi ya wagonjwa 120 wamefanyiwa upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu.

Dk Boniface amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mafanikio ya MOI kwa kipindi cha mwaka mmoja.

"Kabla ya mashine ya ‘angio suite’ haijaja wagonjwa walikuwa anapelekwa nje ya nchi huku gharama za matibabu zikiwa ni Sh milioni 30 hadi Sh milioni 60 lakini hapa ndani ya nchi huduma hiyo ni Sh milioni 10 hadi 15.

Dk Boniface amesema kuwa kupitia huduma hiyo wagonjwa wamekuwa hawakai muda mrefu hospitalini hivyo gharama zinapungua.

"Huduma ya kutoa uvimbe kwenye ubongo unatumia saa moja hadi saa moja na nusu na ndani gharama za kukaa hospitali zimepungua pia ,"ameeleza Dk Bonifane.

Ufungaji wa mashine kwa ajili ya kupasua bila kufungua fuvu (Angio Suite) uligharimu kiasi cha Sh bilioni 7.9 ambapo huduma hiyo ilianza kutolewa Januari 26,2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live