Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI yaanza kutoa matibabu nje ya nchi

MOI Yafanya Upasuaji Wa Kuondoa Uvimbe Kwa Kutumia Pua MOI yaanza kutoa matibabu nje ya nchi

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Tiba ya Ubongo na Mifupa Muhimbili (MOI) imeanza rasmi kutoa huduma maalum ya matibabu kwa wagonjwa wa nje ya nchi na wale wa ndani ya nchi wanaohitaji (International premium care ) ikiwa ni hatua ya kukuza utalii wa matibabu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mkurugenzi wa tiba ya Upasuaji wa Ubongo na Mgongo, Dk. Lemeri Mchome amesema pia wana huduma nyingi bobevu ikiwemo mikono bandi ambao mtu anaweza kufanya kazi kama mkono wa kawaida, unashika akifikiria kuchukua kitu unachukua na kushika vitu mbalimbali kama vile kalamu,gazeti na vingine.

"Tupo kwenye maonesho ya Swahili International export site tunaunga mkono juhudi za serikali katika kupanua tiba au huduma kwenda nje ya mipaka ya nchi na kwa sera ya utalii wa matibabu tumeshafungua tawi la huduma ambapo wagonjwa wanaonywa pale hii ni maalum kwa wagonjwa wa nje na wale wa ndani ambao watahitaji,"ameeleza.

Dk Mchome amesema wanatanua huduma na kufanya kuwa ya viwango vya kimataifa na wanafanya upasuaji wa aina zote za ubongo,mifupa, mgongo na viungo na wamefanya kwa muda mrefu na ni centa kwa Afrika Mashariki na kati huku wakiwa wameendelea kwa kiwango kikubwa.

"Katika kuendeleza tumeendelea kwa kiwango mkubwa sasa tunapasua kwa kutumia njia ya matundu upasuaji huo tunfanya kwenye magoti na tutaenda kwenye Nyonga,kiwiko cha mkono na maega siku za karibuni hatutaweza makovu makubwa,"amefafanua.

Pia amesema wanafanya upasuaji katika mgongo kwa njia ya matundu ambapo mgonjwa anapata nafuu haraka na kukaa mda mfupi hospitali.

Amebainisha kuwa wanafanya upasuaji wa kutoa vivimbe katika ubongo kwa kutumia njia ya matundu kupitia kwenye pua na kutoa uvimbe ambapo pia kuna wataalamu wabobezi.

"Tutaendele kuweka huduma zingine ambazo zinakuwa sawasawa na za ulaya na India kuhakikisha wananchi wanapata tiba nzuri na kuwakusanya wateja kutoka nje,"amesisitiza Dk Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live