Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili, imeshika nafasi ya pili duniani, kwa umahiri wa kutibu wagonjwa waliovunjika mifupa mirefu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali za barabarani.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili, imeshika nafasi ya pili duniani, kwa umahiri wa kutibu wagonjwa waliovunjika mifupa mirefu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ajali za barabarani. Nafasi hiyo ni kutokana na ripoti maalum iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Utengenezaji wa Vifaa Tiba la nchini Marekani linalojulikana kama SIGN Fracture Care International, ambapo imeonyesha kuwa katika mwaka 2023, MOI imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wagonjwa 713 waliovunjika mifupa ya paja(femur) na ugoko(tibia) mwaka 2023, ikiwa nyuma ya Hospitali ya Kossamak ya nchini Cambodia ambayo imefanya upasuaji kwa wagonjwa 1,029.