Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI kuwanoa Madaktari Bingwa

MOI KUWANOA MOI kuwanoa Madaktari Bingwa

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makongamano na semina za mara kwa mara, ili kuendana na maendeleo ya kiteknolojia na uvumbuzi wa mbinu mbalimbali tanzu za kitabibu, zitakazosaidia wakati wa kuwahudumia wagonjwa.

Kauli hiyo wameitoa leo Juni 6, 2023, jijini Dar es Salaam katika kongamano la nane la kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa linaloendelea katika Hosptali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI), lenye lengo la kuwasaidia kujifunza mbinu mbalimbali za matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mifupa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa mifupa sababu kubwa ikiwa ni ajali za barabarani hasa bodaboda, hivyo kongamano hilo kwa kiasi kikubwa linawapa njia ya kupambana na wagonjwa hao.

Naye Mratibu wa Kongamano, Dk Tito Nchimbi amesema ni fursa kwa madaktari bingwa kutoka maeneo mbalimbali kujifunza mbinu mpya za kuwahudumia wagonjwa wenye changamoto hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live