Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MOI, Mnazi Mmoja waanzisha ushirikiano upasuaji mifupa

Upasuaji Madaktari bingwa wa mifupa kutoka Moi na wenzao wa Mnazimmoja wakimfanyia upasuaji nyonga mgonjwa

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Taasisi ya Mifupa (MOI) na hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar zimeanzisha ushirikiano wa kufanya upasuaji wa nyonga na magoti, hatua ambayo itawapunguzia wananchi gharama za kufuata huduma hiyo nje ya kisiwa hicho.

Akizunguma katika kambi ya upasuaji leo Jumamosi Novemba 12, 2022, katika hospitali ya Mnazi Mmoja, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Ahmed Mazrui amesema hiyo ni fursa ya kutibu wagonjwa wengi zaidi kwa gharama nafuu.

“Sio tu itapunguza gharama kwa wagonjwa wenyewe, pia kwa Serikali maana gharama za kumpeleka mgonjwa mmoja India ni sawa na kugharamia watu watano hadi 10 wanaofanyiwa upasuaji huo hapa Zanzibar.

“Mbali na kumpeleka mgonjwa India, hata mgonjwa ukimpeleka Tanzania Bara kwa gaharama za serikali, lakini wapo wagonjwa wanashindwa kumudu hata gharama za malazi, hivyo mtu kuendelea kuteseka,” amesema.

Amesema Serikali imejitayarisha kuona timu zinazotoka Tanzania Bara na nchi nyingine duniani zinapokwenda Zanzibar zikute miundombinu ya kisasa itakayowawezesha kufanya kazi zao kama wanazozifanya katika nchi zao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dk Muhiddin Mahmoud amesema kuwapo kwa kambi hiyo ya siku mbili ni sehemu ya kuadhimisha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Naye Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka MOI, Vailet Lupando amesema kambi hiyo sio tu itawasaidia wagonjwa pekee bali itawaimarisha na kuwaongezea uwezo madaktari wa Zanzibar katika masuala ya upasuaji wa mifupa ambapo wagonjwa 12 wanafanyiwa upasuaji wa magoti, nyonga na kupandikizwa bandia.

Chanzo: Mwananchi