Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MGANGA MKUU: MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA NI VITA

B25800f7fa9ed026b1dd9bb3d3d2cf86 MGANGA MKUU: MAGONJWA YASIYO AMBUKIZA NI VITA

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amesema juhudi za kila mwananchi mmoja mmoja zinahitajika ili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kubadili mtindo bora wa maisha, ulaji wa chakula bora pamoja na kufanya mazoezi.

“Sasa tumeingia katika vita nyingine ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, magonjwa haya hayana dalili ya kukushtua kwenda Hospitali, haya ni hatari zaidi kuliko yale magonjwa ya kuambukiza kama Ukimwi, Kifua Kiuu na hata Malaria” amesema Prof Makubi.

Amesema dalili za magonjwa yasiyo ya kuambukiza huwa hazijitokezi kwa haraka zaidi hivyo mtu huwa anajiona kuwa yuko salama ili hali akiwa mgonjwa ambapo dalili huja baadae kwa uzito mkubwa na mtu huwa amechelewa kuanza kupata matibabu.

Chanzo: habarileo.co.tz