Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAISHA &UHUSIANO : Sababu za watu kuua kwa wivu wa mapenzi

43509 Chris+Mauki MAISHA &UHUSIANO : Sababu za watu kuua kwa wivu wa mapenzi

Mon, 25 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nitaangalia vitu kama vitano ambavyo vitampa mtu uelewa mzuri kuhusu wivu wa mapenzi. Wengi wanadhani wivu wa mapenzi ni mpaka mwanaume au mwanamke wapigane. Watu wanafikiria ukifanya hivyo ndio wivu wa mapenzi.

Wanaangalia zaidi madhara ya kudhuru mwili, lakini yapo mengine ambayo hayazungumzwi sana.

Tofauti ni kwamba wanaume wanaonekana wana wivu zaidi kwa sababu wanachokifanya huwa ni kudhuru, tofauti na wanawake ambao wana wivu mara kwa mara kuliko wanaume, lakini mara nyingi hawadhuru.

Kwanini wanawake hawana madhara makubwa? Kwa sababu wanawake kisaiokolojia ni watu wa hisia, wanawaza kwa hisia, uamuzi wao ni wa hisia, kila kitu hufanya kwa hisia.

Wanaume hawaongozwi kwa hisia, hufanya kitendo baada ya kupata ushahidi tofauti na wanawake ambao anaweza asiwe na ushahidi lakini akalalamika kwa sababu tu amesikia au kuhisi tu.

Wivu wa mapenzi unatoka wapi? Unasababishwa na nini? Mara nyingi wivu husababishwa na ‘social learning’ mambo ambayo mtu hujifunza kutokana na kuona wengine wanachofanya anapokua, anafanya kitu kwa sababu mtu mwingine amefanya.

Wivu wa mapenzi ni kitu ambacho kimeonekana kwenye baadhi ya tafiti kuwa matukio mengi yaliyofanywa kudhuru kutokana na mapenzi, yalifanywa na watu wengi ambao walikuwa wamepata ushawishi wa kilevi, inaweza kuwa kunywa au kuvuta, kujidunga au kunusa madawa ya kulevya.

Mtu hutafuta ujasiri wa ziada kwa sababu yeye mwenyewe hana ujasiri huo. Mara nyingine inaonekana watu wengi kabla ya kufanya hivyo walitumia kilevi kwanza, akiwa tayari na dhamira ingawa anatafutia sababu katika kilevi.

Hatari kubwa ya wivu wa mapenzi ukiangalia kwenye msingi ni kupomoroko kwa maadili au nidhamu ya mahusiano. Tofauti na nyakati za awali, udanganyifu wa mapenzi siku hizi ni jambo la kawaida.

Mtu anadanganya kwa sababu na yeye amedanganywa kimapenzi na anaongea mbele ya wazazi au wakwe bila wasiwasi. Zamani hata kutamka ilikuwa ni ngumu.

Watu wanaangalia madhara ya mwili tu wakati damu imetoka au mtu kachinjwa au kauawa, waangalia hayo tu, wanashindwa kujua kwamba wivu wa mapenzi unaweza kuleta madhara ya mwili, nafsi pia inaweza kudhuriwa.

Mfano umemshusha hadhi mwenzi wako, umezira au kumnyima tendo la ndoa, au kununa au kuhama nyumbani, hicho kitendo umefanya lakini hujampiga mtu, hajashika mapanga, hujamshkia kisu, hujampiga lakini tayari umemsababishia majeraha ya hisia.

Na baadhi ya watu wanasema kwamba majeraha ya hisia ni makubwa au endelevu kuliko yale ya mwili.

Kuna kitu kinaitwa mfumo dume, mwanaume anaweza kudanganya kimapenzi mara tatu au zaidi, mwanamke akiuliza amsamahe, mwanamke licha ya kuonekana tu hata kama hajadanganya anaweza kuuawa.



Chanzo: mwananchi.co.tz