Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAISHA NA UHUSIANO: Aina 10 za wake

47085 PIC+UHUSIANO

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara nyingi kwenye ndoa kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wanaume na yanaelekezwa kwenye namna wake zao wanavyoishi au wanavyofanya. Huyu analalamika mke wangu yuko hivi, na yule naye anasema wangu yuko vile.

Mmoja anasema mke wangu anafanya hivi na mwingine analia hafanyi vile. Huu mkanganyiko umekuwa mkubwa sana na unasababisha maumivu na migongano kwenye ndoa nyingi.

Hii ndio maana nimeamua kuna na makala hii itakayokusaidia kufahamu kuwa wake zetu pamoja na kwamba wanafanana kijinsia lakini kwenye tabia zao katika ndoa wanatofautiana sana.

Labda kwa kuisoma makala hii utajigundua kuwa wewe ni mke wa aina gani (kama wewe ni mke) na labda pia utamgundua mke wako yuko kundi gani.

Mke sherehe

Wake wa aina hii wako mguu na njia kila siku na wanajuana na kila mtu. Wao kila siku wana sherehe, leo sendoff, kesho kichen party, keshokutwa bag party mtondogoo harusi. Mara chache wanakaa nyumbani siku za wikiendi, yaani zile siku za mume na watoto kuwepo nyumbani yeye ndio anakuwa na mshawasha wa sherehe. Wanaweza kutumia hela ya chakula cha familia kuchangia sherehe au kununulia zawadi.

Mke kamusi

Hahitaji kuomba ushauri hata siku moja yeye anachojua ndio mpango mzima. Kila wakati analazimisha mawazo yake yawe sawia na yaaminike. Hataki kupingwa au kurekebishwa kwa chochote. Anatoa oda tu, neno naomba au tafadhali hutolisikia kwake, na ni mkali sana vitu vinavyopotea au kuwekwa vibaya nyumbani tofauti na alivyovipanga yeye.

Mke pampas

Huyu ni mke aliyeharibiwa kabisa na wazazi wake hususani wazazi matajiri, wanaojiweza, au labda ndio binti pekee kwao. Wavivu sana kufanya kazi za nyumbani. Wao wanapenda tu kufanya manunuzi na vitu vya fasheni. Mara nyingi mke huyu anamwona mume wake kama kijakazi, utasikia baby nisaidie hiki, baby niletee kile, hubby njoo nitolee hiki, hubby utanipeleka pale. Mume utadhani dereva au shamba boy. Unakuta mume ana hasira moyoni lakini ndio hivyo tena kamba ilishaungulia kiwandani.

Mke ofisi

Mke wa aina hii anajali sana majukumu ya kazini kuliko familia yake, anaweza kuwa na muda mrefu sana wa kazi akakosa muda na watoto au mume wake na anatumia majukumu ya kazi kama kisingizio cha kutokuwepo nyumbani au kutotimiza majukumu yake ya mke au mama nyumbani.

Ni ngumu sana kwa mke wa hivi kumheshimu mume wake na hawa ndio wanaowafanya wanawake wengine waliosoma kuonekana wabaya kwenye ndoa.

Mke mgonjwa

Wakati wote anaonekana kama anaumwa, mpole sana na aliyenyong’onyea. Anapenda kulaumu kila kitu, atalaumu kuhusu mume, watoto, ndugu hata hali ya hewa.

Kila wakati wao ni wenye hofu kwa kila kitu, ukimshauri afanye bishara hii anaogopa mwambie nyingine ataogopa, anaweza kulalamika uchovu au kuumwa hata katika nyakati mume anaomba tendo la ndoa. Pamoja na lawama za udhaifu na kuumwa au kuchoka mara kwa mara wala hauoni akisema anaenda hospitali.

Itaendelea…..



Chanzo: mwananchi.co.tz