Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MAISHA NA KISUKARI: Upungufu wa nguvu za kiume kwa wenye kisukari

59403 Pic+sukari

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ugonjwa wa kisukari ni miongozi mwa sababu za ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume.

Unaweza ukajiuliza kuna uhusiano gani kati ya kisukari na upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume?

Tatifi mbalimbali za afya zinaonyesha kuwa asilimia 55 ya wanaume wenye kisukari hupatwa na tatizo la nguvu za kiume.

Endapo kiwango cha sukari kwenye damu kikiwa juu kuliko kawaida huweza kusababisha madhara mengi sana mwilini, kama vile figo, moyo, shinikizo la damu, ulemavu wa viungo na upofu.

Pia, huathiri mfumo na mishipa ya fahamu, damu na hurudisha nyuma uchumi wa nchi kwa sababu huongeza watu wenye ulemavu na katika matibabu pia ni gharama kubwa.

Kwa upande wa afya ya mfumo wa nguvu za kiume, lazima ubongo uwe imara na wenye afya, mishipa ya damu na fahamu iwe katika afya njema.

Pia Soma

Mishipa na misuli ya uume lazima iwe katika afya njema na imara, kusiwe na hitilafu yoyote katika mishipa ya fahamu iliyo katika ubungo, uti wa mgongo na misuli mingine muhimu katika mfumo wa uume.

Sukari nyingi katika damu huweza kusababisha uharibifu kwenye kuta za mishipa ya damu; kisha kuta hizi hushindwa kuzalisha homoni aina ya Nitrogen Oxide ambayo husaidia kutanua mirija ya damu kwa ajili ya kupitisha damu kwa urahisi.

Ikitokea hali hiyo mirija ya damu hushidwa kutanuka vizuri, hivyo uume hupungua uimara wake na kushindwa kufanya kazi.

Kama kisukari kitashambulia sehemu tajwa hapo, ndipo tatizo la ukosefu au upungufu wa nguvu za kiume hutokea.

Wanaume wengi wenye kisukari ambao wamepata tatizo la nguvu za kiume hukimbilia katika matumiza ya dawa za kuongeza nguvu za kiume.

Kwa mgonjwa wa kisukari dawa hizi huweza kusababisha matatizo mengine kama shinikizo kubwa la damu.

Chanzo: mwananchi.co.tz