Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya utamu wake, nanasi lina faida hii

82636 Nansi+pic Licha ya utamu wake, nanasi lina faida hii

Mon, 4 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwili unapokosa kinga imara, unakuwa katika hatari ya kushambuliwa na kila aina ya magonjwa, lakini nanasi lina sifa ya kukabilina na hali hiyo.

Nanasi ni moja kati ya matunda yenye vitamini, madini na virutubisho vingi vinavyoupa mwili nguvu na kuepuka kushambuliwa na madhara.

Herieth Nyange ni Ofisa Lishe wa Mkoa wa Dodoma, anasema ulaji wa tunda hili mara kwa mara, utasaidia kuupa mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali hasa pumu na shinikizo la damu.

Mtaalamu huyo anase ma ili upate kinga dhidi ya maradhi mbalimbali, mtu anashauriwa kula tunda hilo kabla au baada ya kula mlo wake.

Anafafanua kuwa tunda hilo lina virutubisho vingi ikiwamo vitamin A, B na C na ina madini ya chuma, calcium na phosphorous na potasium, ambayo ni muhimu katika afya ya binadamu.

“Katika nanasi kuna makapimlo ambayo husaidia mmeng’enyo wa chakula, lakini calcium iliyopo husaidia kuimarisha afya ya mifupa na meno,” anasedma Nyange. Pia, anasema mbali na faida hizo, nanasi linakabiliana na magonjwa ya moyo kutokana na vitamini C na potasium iliyopo ndani yake.

“Wagonjwa wenye matatizo ya pumu, wanashauriwa mara nyingi kula nanasi kwa sababu lina vitamini ijulikanayo kama beta caroti, ambayo husaidia mwili kukabiliana na magonjwa,” anasema Nyange.

Chanzo: mwananchi.co.tz