Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwimba yajipanga kupunguza Usambaaji wa VVU kwa vijana

385fd400ae6ac129f783cdc69ec5c623 Kwimba yajipanga kupunguza Usambaaji wa VVU kwa vijana

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza ipo katika mikakati ya kuhakikisha inaendelea na juhudi za kupunguza kasi za maambukizi ya virusi kwa Ukimwi kwa vijana.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Elimu ya Ukimwi kwa vijana,Mratibu wa Ukimwi wilaya ya Kwimba Dk Ally Sadik alisema wilaya yao jumla ina watu wanaotumia tumia dawa za kupunguza makali ya virusi(ARV) 13,268 kwa takwimu za Septemba 2020. Alisema vifo vitokanavyo na ugonjwa huo in 1622 huku vijana idadi ya vifo vyao ni 1050 ambapo ni sawa na asilimia 67% na kwa watoto ni 210.

Alisema kuna vifo 8842 vya watu wenye umri wa miaka 25 mpaka 49.

Dk Sadik alisema mwaka 2017 maambukizi yalikuwa asilimia 1.6% na sasa ni asilimia 4.8%. Alisema wilaya yao ina jumla ya vituo 39 ambavyo vinazuia maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mama na mtoto.

Alivitaja vituo hivyo ambavyo ni Hospitali za Sumve na Ngudu,pamoja na vituo vya Afya vya Nyambiti,Malya,Nyamilama na Mwanashimba. Alisema katika jitihada za kupambana na VVU wamefanikiwa kufungua vituo vya Tohara kwa Wanaume katika vituo vya Ngudu,Bujingwa,Nyamikoma na Malemvi.

Alisema kupitia Tohara inapunguza asilimia asilimia 60 ya kupata maambukizi.Mratibu wa mradi huo wa vijana kutoka hospitali ya Sumve,Sebastian Gregory alisema asilimia kubwa ya vijana kati ya miaka 15-24 wanaishi na VVU hivyo mradi wa utawahimiza utumiaji wa sawa za ARV.

Alisema mradi wao utanufaisha shule 20 wilayani humo ambapo baadhi ni shule ya Sekondari Sumve,Mwashilala,Mantare,Bungolwa,lwala na Mwabomba. Mradi huo wa utoaji wa Elimu ya Ukimwi kwa vijana unadhaminiwa na Ambassador’s Fund for HIV/AIDS Relief.

Chanzo: habarileo.co.tz