Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwanini ulevi huwaathiri zaidi wanawake?

75670 POMBE+PIC

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miezi michache iliyopita Shirika la Afya Duniani, (WHO) lilifanya tafiti zake na kuhitimisha kuwa, kiwango chochote kile cha pombe si salama kiafya.

Hivyo, ni vyema ikaeleweka kuwa unywaji wa pombe kwa ujumla wake ni hatari kwa afya hata kama ikitumika kwa kiwango kidogo. Lakini tafiti hizi hazikushia hapo, siku chache zilizopita tumepokea tena ripoti kutoka WHO kuwa, madhara ya pombe yanatofautiana kulingana na jinsia, yaani inawaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume.

Kisayansi kuna sababu nyingi zinazosababisha pombe kumuathiri zaidi mwanamke kuliko mwanamume na baadhi ya sababu hizi ni kama ifuatavyo: Kwanza kabisa ifahamike kuwa kisayansi, wanawake wana kiwango kidogo cha maji mwilini kuliko wanaume. Tofauti na kimo au uzito, wanawake wana sehemu kubwa ya mafuta (fat) katika miili yao wakati wanaume wana sehemu kubwa ya ujazo wa misuli kwenye miili yao.

Mafuta yana mkusanyiko wa asilimia 25 tu ya maji wakati misuli ina mkusanyiko wa asilia 75 ya maji. Kutokana na dhana hii, wanawake wana kiwango hafifu cha maji mwilini tofauti na wanaume. Wakati pombe inaponywewa na kuingia mwilini, inachakatwa na kile kiwango cha maji kinachobaki baada ya kuchunjwa kwenye mfumo wa mkojo kinaingia kwenye mzunguko wa damu. Sasa kwa sababu wanawake wana kiwango hafifu cha maji cha kuweza kuzimua ile pombe, inaingia mwenye mikondo ya damu na hivyo kusababisha damu inayozunguka mwilini kuwa na uwepo wa kiwango kikubwa cha pombe na hata kusababisha pombe kudumu kwa muda mrefu mwilini tofauti na wanaume. Pia, sababu nyingine, mwilini kwenye mfumo wa chakula, kuna kimeng’enya ambacho kitaalamu kinaitwa “Enzyme Alcohol Dehydrogenase.”

Kimeng’enya hiki ni maalumu kwa ajili ya kuvunja vunja yakula vyote ambavyo vimeambatana na kiwango chochote kile cha pombe kabla pombe haijaingia kwenye mikondo ya damu. Sasa kisayansi kimeng’enya hiki ni hafifu na dhaifu zaidi kwa mwanamke kuliko mwanamume, hivyo kusababisha kiwango kikubwa cha pombe kuingia kwenye mikondo ya damu kuliko ya damu. Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz