Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini wanawake hupata tatizo la kutofika kileleni?-2

82639 Dk+Shita+Samwel Kwa nini wanawake hupata tatizo la kutofika kileleni?-2

Mon, 4 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wiki iliyopita katika makala haya nilieleza kuwa kufika kileleni au kufika mshindo ni tukio linahusisha upitaji wa hatua kadhaa wa usisimuliwaji wa kimwili na kiakili.

Kwa kitabibu kufika mshindo kunajulikana kama orgasm na kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama ‘coming’ au ‘climaxing.’

Mwanamke kufikishwa kileleni na kuridhika ni jambo linalohitaji ushirikiano na kuelewana kwa wenza wawili wanaoshiriki tendo hilo hasa katika maandalizi ya awali.

Kutofika kileleni kwa mwenza yoyote ni moja ya mambo yanayochangia migogoro isiyo na lazima kwani baadhi hudhani kuwa mwenza wake si mwaminifu katika mahusiano yao.

Kufika kileleni kwa baadhi ya wanawake huambatana na kutoa maji maji yanasukumwa ukeni kwa kasi ambayo si haja ndogo kama inavyodhaniwa mitaani.

Kwa kawaida maji hayo hutokea ndani ya tezi ambayo mdomo wake upo jirani na tundu la njia ya haja ndogo. Tezi hiyo hujulikana kama tezi ya Skene, ndani yake huwa na maji maji meupe. Kwa upande wa wanaume, kufika kwao kileleni huambatana na kupata hisia nzuri za kipekee na kutoa maji maji mazito ambayo huwa yana mbegu za kiume.

Hisia hizi huweza kudumu kwa sekundi 6-30 na huwa ni mara moja tu na si mfululizo kama ilivyo kwa mwanamke. Huitaji muda kidogo ila kuamsha tena hisia na kuendelea na tendo na kufika kileleni tena.

Wapo baadhi ya wanaume baada ya kufika kileleni katika mzunguko wa kwanza wanauwezo wakuunganisha kwenda mzunguko wa pili bila kuhitaji mapumziko mafupi na kufika kileleni kwa mara ya pili. Yapo mambo kadhaa yanaweza kuchangia mtu asifike kileleni ikiwamo matatizo ya kiakili kama vile hasira, woga, hofu, wasiwasi na kuumizwa kihisia.

Vile vile majeraha katika maeneo ya uzazi ikiwamo kukeketwa, kujeruhiwa wakati wakujifungua, kupata ajali na kujijeruhi maeneo ya uzazi na uwapo wa magonjwa sugu mwilini.

Epuka kuona aibu fika katika huduma za afya kwa ushauri na matibabu.

Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

Chanzo: mwananchi.co.tz