Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini unashauriwa kunywa supu ya mchele?

63843 Mchele+pic

Sat, 22 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Licha ya mchele kutumika katika matumizi ya mapishi, lakini wengi hawafahamu kama unaweza kupika supu.

Kama ulikuwa hujui supu ya mchele, basi leo hii utaweza kujua faida ya supu ya mchele kwa afya.

Supu ya mchele husaidia kuboresha umeng’enywaji wa chakula na kumsaidia mtu anayeharisha.

Ofisa Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Julieth Shine anasema supu ya mchele (wali) inaweza kutumiwa na watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) na wenye Ukimwi kwa sababu mara nyingi hupata matatizo ya ulaji, umeng’enywaji na ufyozwaji wa chakula mwilini.

Shine mchele ni aina ya nafaka inayotokana na punje ya mpunga.

Zao hilo hulimwa katika nchi za Asia na Afrika katika maeneo yanayopata maji mengi ya mvua na yale yanayotuama katika maeneo yenye mabonde.

Pia Soma

Shine anasema baada ya kuvunwa mpunga, hukobolewa na kisha hupatikana mchele ambao hutumika kama chakula.

“Matumizi ya mchele kama chakula ni maarufu sana; wengi hupika wali, ubwabwa, pilau na madida,” anasema Shine.

Namna ya kuandaa supu ya mchele

Mtaalamu huyo anasema chukua mchele kikombe kimoja, kitunguu saumu kikonyo kimoja, unga wa mdalasini kijiko kimoja cha chai, chumvi kidogo na maji vikombe vitano.

Baada ya hapo, chemsha mchele, ongeza kitunguu saumu, mdalasini na chumvi kiasi kisha funika na pika taratibu hadi vilainike, pia unaweza kuongeza karoti au boga lililokwaruzwa (boga lililokwanguliwa).

Anasema baada ya kuiva mchanganyiko huo, mtu anaweza kunywa kikombe kimoja kutwa mara nne kwa siku.

Makala haya yameandikwa na mwandishi wa gazeti hili HadijaJumanne.

Chanzo: mwananchi.co.tz