Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa nini ukatili, unyanyasaji kazini wahitaji mwarubaini

6ccde6207fe8fafb5ea41bd101b2fd00 Kwa nini ukatili, unyanyasaji kazini wahitaji mwarubaini

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAZI ni muhimu kwa maisha ya watu. Kazi ni uhai na hata maandiko matakatifu, kama yalivyokuwa yakinukuliwa na Hayati Rais Johh Magufuli, yanasema kwamba “asiyefanya kazi na asile”.

Je, kila wakati watu wanafanya kazi katika katika mazingira sahihi na yasiyo hatarisha katika maisha yao? Je, kazi wanazofanya ni za staha? Haki zao kama wafanyakazi zinaangaliwa ipasavyo na waajiri?

Hakuna manyanyaso? Ni kutokana na hayo, mara kwa mara Shirila la Kazi Dunia (ILO) limekuwa likija na maazimio na mikataba ambayo inatarajia mataifa yote kuridhia mikataba hiyo kwa sababu ipo katika kuhakikisha ulimwengu wa kazi unakuwa bora zaidi.

Kwa mfano, Agosti 2013, ILO ilikuja na mktaba wa kimataifa kuhusu ajira za wafanyakazi kwenye vyombo vya majini, mwaka 2014 Shirika hilo likaja na na mkataba wa kisheria uliolenga kuimarisha juhudi za kimataifa za kuzuia na kutokomeza ajira za kulazimishwa pamoja na utumwa wa kisasa.

Lakini mwezi Juni mwaka juzi, 2019, Shirika hilo limekuja na mkataba mwingine muhimu sana, Mkataba namba C190 unaojielekeza katika kupambana na ukatili au dhulma na unyanyasaji mahala pa kazi ambao makala haya yanauangazia kwa kina.

Likiwa na lengo la kuhakikisha kwamba mkataba huu unafahamika kwa watu ili hatimaye ikiwezekana nchi yetu iufanyie kezi na kuuingiza kwenye sheria zetu, Shirika la Actionaid, lilifanya semina kwa waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam ili waufahamu mkataba huo na umuhumu wake.

Matarajio ya semina hiyo ni waandishi kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi wakiwemo watunga sera kuhusu mambo muhimu yaliyomo kwenye mkataba huo ili wachukue hatua kadri itakavyoonekana inafaa.

Ni nini kilichomo kwenye mkataba huu? Katika semina hiyo, waandishi walijifunza kupitia kwa mtoa mada, Wakili wa Kujitegemea, Anney Nahum, kwamba ni mkataba unaohakikisha haki ya kila mtu ulimwenguni kufanya kazi bila dhulma na udhalilishaji na kufanya kazi bila unyanyasaji wa kijinsia.

Vitendo vya ukatili Mkataba hauhusu vitendo vya ukatili wa kimwili pekee bali unafafanua dhulma na unyanyasaji kama tabia na mazoea yasiyokubalika na yasiyo na chembe ya uadilifu.

Matendo hayo ni pamoja na vitisho, iwe vimefanywa mara moja au mara kadhaa ambavyo vinalenga au kuweza kusababisha madhara kimwili, kisaikolojia, kijinsia au kiuchumi.

Vitendo hivyo ni pamoja na vinayohusiana na dhulma au ukatili wa kijinsia. Vitendo hivyo vinaweza kujumuisha unyanyasaji wa kimwili na matusi ya maneno, ukatili, unyanyasaji wa kijinsia, vitisho au maneno yenye kuogofya, kudunisha na kudhalilisha, kufanyiwa hila pamoja na mazoea ya kazi yanayonyanyasa na kusababisha madhara mwilini, kisaikolojia, kijinsia au kiuchumi.

Vitendo kama hivi vinaweza kupunguza kasi ya uzalishaji kwa mhusika au huweza kumsababishia mfanyikazi maumivu, majeraha au madhara ya kiuchumi.

Unyanyasajiwa kijinsia Mkataba huo unafafanua kwamba ukatili na unyanyasaji wa kijinsi ni vitendo vinavyohusu vurugu na dhuluma zinazoelekezwa kwa mtu kwa misingi ya jinsi yake, au hali ya kuathiri watu wa jinsi fulani kwa njia ya upendeleo.

Huku sehemu kubwa ya waajiri au mameneja makazini wakiwa na wanaume, ukatili na udhalilishaji umekuwa ukifanywa zaidi dhidi ya wanawake kuliko wanaume.

Hii ni pamoja na wanawake kuombwa rushwa ya ngono ili wapate haki fulani kazini, wanawake kuachishwa kazi au kutoajiriwa kwa sababu ya ujauzito, kudharauliwa kwa sababu tu ni wwanamke na mengine mfano wa hayo. Je, ni nani analindwa na mkataba huu?

(Itaendelea).

Chanzo: www.habarileo.co.tz