Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa mara ya kwanza wabobezi JKCI wapandikiza kifaa kuusaidia moyo

333709e5d7cd3df3fd9ffd9c2c98157b Pacemaker

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Kwa mara ya kwanza wataalamu wabobezi wa moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepandikiza kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Pacemaker) nje ya taasisi hiyo bila ya kutumia mtambo wa Cathlab, Imeelezwa.

Mgonjwa aliyewekewa pacemaker alipata ajali iliyosababisha uti wa mgongo kupata shida na kusababisha baadhi ya viungo vya mwili kupoteza uwezo wa kufanya kazi ikiwemo mishipa ya damu  inayoratibu uwezo wa moyo kutengeneza mapigo yake (Sympathetic Waves System).

Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI Yona Gandye alisema kutokana na tatizo alilolipata mgonjwa huyo mara baada ya kupata ajali mapigo ya moyo yalishuka hadi kufikia 30 kwa dakika na mgonjwa kuonesha dalili za ukosefu wa mahitaji muhimu ya mwili yanayosambazwa na mapigo ya moyo ambayo  ni oxygen , virutubisho, madini na chakula.

"Mgonjwa huyo alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na alihitaji huduma ya haraka ya kuwekewa kifaa kisaidizi ambacho kinausaidia moyo kufanya kazi vizuri (Pacemaker)  ili mapigo yafikie 60 hadi 100 ambayo ni mapigo ya kawaida ya moyo,” alieleza daktari huo.

...

Kwa taarifa zaidi, soma gazeti la Habari Leo kesho Jumamosi.

Chanzo: habarileo.co.tz