Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwa dalili hizi, unanyemelewa na kisukari-2

73495 Kisukari+pic

Fri, 30 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mara kadhaa tumekuwa tukiangukia kwenye maradhi mbalimbali makubwa yasiyoambukiza kutokana na kuzipuuzia dalili za awali.

Hali hiyo husababisha kupata matibabu wakati ambao tatizo limeshakuwa kubwa na siyo rahisi tena kutibika.

Magonjwa kama saratani, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kisukari ni baadhi tu ambayo yasipobainika na kudhibitiwa kwenye hatua za awali, huleta madhara makubwa sana kiafya na hata kusababisha kifo. Njia pekee ya kuyadhibiti magonjwa haya ni kupata vipimo vya mara kwa mara na kutozipuuzia dalili za awali. Ni matumaini yangu kuwa angalau unauelewa kuhusiana na ugonjwa huu. Miili yetu inahitaji kiwango fulani cha sukari kwa kuwa kina kwenye afya zetu lakini ikizidi au kupungua, huleta tatizo.

Kuwa makini sana na kupata haja ndogo kupita kiasi na kiu iliyopitiliza. Kwa kawaida, figo hufanya kazi ya kuchuja malighafi zote zilizo katika hali ya kimiminika mwilini, baada ya mchakato huu, figo huzisababisha malighafi safi zitumike mwilini na zile chafu zitoke nje ya mwili kupitia haja ndogo.

Sasa ikitokea kiwango cha glucose yaani sukari kimezidi kwenye damu, figo hushindwa kufanya kazi yake ya kuchuja malighafi hizi kikamilifu, hivyo kusababisha kiwango kikubwa cha maji kupotea mwilini.

Na hapa ndipo wakati ambao mgonjwa huwa anapata haja ndogo kupita kiasi, hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha maji kutoka bila kuchakatwa kwa sababu tayari figo zinashindwa kufanya kazi vizuri kwa kuwa zimeathiriwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.

Pia Soma

Advertisement   ?
Kutokana na kukojoa kupita kiasi, mtu husikia kiu mara kwa mara kwa kuwa kiwango cha maji kinachotoka nje ya mwili ni kikubwa.

Dalili nyingine ya kisukari ni kuanza kupoteza uwezo wa kuona vizuri. Watu wengi wanapoanza kupata matatizo ya kuona wanakimbilia kwa wataalamu wa macho ili kupewa miwani. Hili ni kosa. Takribani asilimia 40 ya kesi za macho husababishwa na kisukari.

Mishipa ya kwenye jicho ikishaathiriwa na sukari, mtu huanza kuona ukungu, kushindwa kuona mbali. Hivyo upatapo tatizo la kuona ukungu au kutoona mbali; ni vyema ukachunguzwa kwanza kisukari kabla ya kwenda kutafuta miwani. Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

Chanzo: mwananchi.co.tz