Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kutengeneza shepu na kwa waliokoma kuzaa tu

Mloganzila Upasuaji Makalio Kutengeneza shepu na kwa waliokoma kuzaa tu

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WANAWAKE wanaotaka kufanya upasuaji wa kuboresha maumbile yao ikiwemo kutolewa mafuta tumboni ‘Tummy Tuck’ na kuwekewa kwenye mapaja na maeneo mengine ya mwili wameshauri kumaliza kuzaa kwanza kabla ya kukimbilia huduma hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Daktari bingwa wa magonjwa rekebishi na sanifu, Edward Wayi, kutoka hospitali ya CCBRT jijii Dar es Salaam katika mahojiano maalum na HabariLeo.

Amesema, CCBRT wanatoa huduma hiyo kwa mama ambaye haitaji kubeba tena ujauzito.

“Mwanamke ambae haitaji tena kuzaa ndio tutamkubali kumfanyia upasuaji kwa ajili ya kupunguza tumbo ‘Tummy Tuck’ hatutarajii tena aje kubeba ujauzito,”amesema na kuongeza

“Ukishafanya ‘Tummy Tuck’, ni ngumu kubeba ujauzio kwa kuwa nafasi ya tumbo litakuwa ni ndogo hivyo itakuwa ni changamoto kubwa.

Aidha, amesema hata wanawake wanaokwenda kufanya usanifu wa matiti ama yawe makubwa au madogo nao wawe wamemaliza zoezi la kunyonyesha.

“Mama anayehitaji kupunguza maziwa yake tunashauri awe amemaliza kunyonyesha yaani kwamba hana mpango wa kuzaa tena huyo tutamkubali na kumfanyia upasuaji sanifu,

“Tunavyofanya upasuaji wa kuboresha matiti tunapunguza kiasi kikubwa cha vichocheo vya kuzalisha maziwa, hivyo zikiwa zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa tunatarajia kwamba kama amepata ujauzito upo uwezekano mdogo sana wa kuzalisha maziwa, ndio maana tunashauri awe amemaliza zoezi la kuzaa." Amesisitiza bingwa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live