Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuna umuhimu kwa wanaume kuzingatia uzazi wa mpango

39819 Pic+uzazi Kuna umuhimu kwa wanaume kuzingatia uzazi wa mpango

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tofauti na ilivyo miaka ya nyuma, utoaji wa mimba zisizopangwa na uzaaji holela usiofuata utaratibu wa uzazi wa mpango umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi ya njia za uzazi wa mpango.

Njia hizi za uzazi wa mpango zimeleta tija katika familia nyingi japo pia kama daktari nakiri kuwa bado elimu zaidi inahitajika itolewe ili wazazi wapate uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa ujumla wake.

Hata hivyo, suala la matumizi ya njia za uzazi wa mpango linaweza kuibua maswali kadha wa kadha na kuleta mdahalo kwenye jamii zetu, na maswali haya wakati mwingine huwa tunakuta nayo sisi wahudumu wa afya; na baadhi ya maswali yanayoleta mjadala ni kama vile;

•Je matumizi ya njia hizi mbalimbali za uzazi wa mpango zinazingatia usawa wa kijinsia?

• Njia hizi za uzazi wa mpango ni rafiki kwa afya ya mtumiaji? (hasa mwanamke kama ilivyozoeleka)

Maswali mengi yanayohusiana na matumizi ya njia za kupanga uzazi huwa yanalenga maeneo haya mawili lakini leo nitajikita kueleza kuhusiana na usawa wa kijinsia.

Tendo la ndoa, na hasa linalofanywa bila kutumia kinga, mara nyingi linakuwa na matokeo mawili. Matokeo haya ni magonjwa mbalimbali ya zinaa na mimba. Lakini hii haimaanishi kuwa kila washiriki wanapofanya tendo la ndoa bila kutumia kinga wanapata mambo haya kwa pamoja hapa! Wanaweza wakapata moja tu ya mambo haya, au wasipate kabisa. Itategemea tu wapo hatarini kiasi gani kupata moja ya mambo haya au yote kwa pamoja.

Suala la kujikinga au kuzuia magonjwa ya zinaa imezoeleka kuwa ni jukumu la wote wawili yaani mwanaume na mwanamke wake, lakini suala la kuzuia mimba na kupanga uzazi wengi wanadhani kuwa ni jukumu la mwanamke.

Na ndio maana inapofikia kwenye suala la kupanga uzazi mzigo wote wa kutumia njia mbalimbali za kupanga uzazi unabaki kwa mwanamke. Nina imani kuwa wengi wanadhani ya kuwa, wanaume nao hawana njia zao za uzazi wa mpango, la hasha! Wanaume nao wana njia zao za kupanga uzazi, na wakizitumia kwa usahihi zinaweza kuleta matokeo chanya hata kama wanawake au wapenzi wao wa kike wasipozitumia.

Hivyo nina imani wanaume kuanzia sasa mtaanza kuzingatia njia za uzazi wa mpango kwa lengo la kuwasaidia majukumu wanawake wenu kama nitakavyoeleza.

Kuchunga kalenda, ni njia rahisi na ya asili ambayo mwanamke anaweza kuitumia katika kupanga uzazi, lakini njia haijaonekana kutumiwa na wanawake wengi kutokana na kuwa ngumu, hivyo wanawake wengi hutumia njia mbadala kama vile vidonge, vitanzi, sindano na vinginevyo.

Kisayansi, pamoja utendaji kazi wa njia hizi, lakini bado zimeonekana kuleta madhara mengine ya kiafya na madhara haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu.

Kuvurugika kwa mfumo wa homoni na mzunguko wa hedhi, hedhi iliyopitiliza au kukosa kabisa hedhi, maumivu ya tumbo, kiuno na mgongo wakati wa hedhi, na kupata uzito wa mwili uliopitiliza ni baadhi tu ya matatizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz