Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kulala kabla ya saa 4 usiku ni chanzo cha magonjwa ya Moyo

95029 Moyo+pic Kulala kabla ya saa 4 usiku ni chanzo cha magonjwa ya Moyo

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tafiti za kisayansi zimeonesha kwamba kuna muda muafaka wa kulala - kati ya saa 4 na 5 usiku - ambao unaohusishwa na afya bora ya moyo, wanasema watafiti ambao wamewachunguza watu 88,000 waliojitolea takribani.

Timu maalumu kutoka Biobank ya Uingereza inaamini kwamba kuwa na uwiano sawa wa usingizi na namna mwili unavyotaka kunaweza kufafanua uhusiano uliopo wa uwezekano wa kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo pamoja na kiharusi.

Namna ya mwendendo wa asili wa mwili wa saa 24 ni muhimu kwa ustawi pamoja na tahadhari. Kwa sababu kuna uwezekano wa kutokea kwa shinikizo la damu.

Katika utafiti huo, ambao umechapishwa katika Jarida kuhusu masuala ya Moyo la Ulaya, watafiti walikusanya data kuhusu nyakati za kulala na kuamka kwa zaidi ya siku saba kwa kutumia kifaa kinachofanana na saa ya mkono kinachovaliwa na watu waliojitolea.

Walifuatilia kile kilichotokea kwa waliojitolea katika suala la afya ya moyo na mzunguko wa damu kwa wastani wa miaka sita.

Zaidi ya watu wazima 3,000 walipata ugonjwa wa moyo na mishipa. Visa hivi ving kati ya zilizotokea kwa watu ambao walichelewa kulala au walilala mapema kabla ya muda muafaka wa kati ya saa 4 na saa 5 usiku.

Watafiti hao walijaribu kudhibiti vyanzo ama mambo mengine yanayosababisha matatizo ya moyo wa mtu, kama vile umri wao, uzito na viwango vya 'cholesterol', lakini mkazo uliowekwa na utafiti wao ni kwmaba hauwezi kuthibitisha chanjo na athari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live