Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kula vyakula hivi uone faida yake

68461 Vyakula+pic

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Upungufu wa madini chuma ni tatizo kwa wakazi wa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania.

Hata hivyo, upungufu wa madini hayo husababisha upungufu wa wekundu wa damu na hatimaye upungufu wa damu mwilini.

Tatizo hilo linaweza kukabiliwa kwa mtu kula vyakula vya asili ya wanyama na mimea, vinavyoongeza madini hayo.

Nyamizi Ngassa ni Ofisa Lishe Mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe(TFNC) anasema vyakula vya asili ya wanyama vina madini chuma yanayoweza kufyonzwa kwa urahisi mwilini.

Anasema madini chuma hupatikana kwa wingi zaidi kwenye nyama za ndani kama vile maini, figo, moyo na nyama nyekundu. Pia, vyakula vingine ni dagaa, samaki na nyama ya kuku.

Ngassa anavitaja baadhi ya vyakula vyenye asili ya mimea vyenye madini chuma kwa wingi kuwa ni mboga zenye rangi ya kijani mfano matembele, mnavu, mchicha, kisamvu na mlenda. “Ulaji wa matunda yenye vitamini C husaidia ufozwaji wa madini chuma kutoka kwenye vyakula vyenye asili ya mimea mfano ubuyu, ukwaju, machungwa, choya (rozela),” anasema.

Pia Soma

Mtaalamu huyo wa lishe anasema hapa nchini, tatizo la upungufu wa wekundu wa damu (anemia) linawakabili sana watoto chini ya umri wa miaka mitano, wajawazito, wanawake waliokatika umri wa kuzaa (kuanzia miaka 15-49) na vijana balehe.

“Kwa mujibu wa takwimu za afya na demiografia Tanzania ( TDHS 2015/2016); asilimia 58 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano wana upungufu wa wekundu wa damu,”anasema Ngassa.

Muhimu

Ngassa anasema ulaji wa matunda yenye uchachu kama vile machungwa, ubuyu, ukwaju vikiliwa pamoja na mlo husaidia ufyonzwaji wa madini chuma kwenye chakula.

Angalizo

Unywaji wa chai, kahawa na ngano isiyokobolewa pamoja na baadhi ya mboga za majani kama vile kabeji vinazuia ufyonzwaji wa madini chuma mwilini hivyo inashauriwa kutokula au kunywa pamoja na mlo.

Ngassa anashauri wajawazito watumie vidonge vya madini chuma na asidi ya folic kila siku katika kipindi chote cha ujauzito na miezi mitatu baada ya kujifungua.

Makundi mengine kama vile watoto, vijana balehe na watu wazima wazingatie ushauri wa wataalamu wa afya wakati wa kutumia vidonge vya madini chuma na asidi ya folic.

Makala haya yameandikwa na mwandishi wa gazeti hili Hadija Jumanne.

Chanzo: mwananchi.co.tz