Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kudhibiti ulaji kunasaidia matibabu ya saratani-Utafiti

69526 Pic+ulaji

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kudhibiti ulaji, tayari ni sehemu muhimu ya kukabiliana na magonjwa kama kisukari na shinikizo la damu, lakini utafiti mpya unaongeza ushahidi unaokua kwamba jambo hilo pia linaweza kusaidia matibabu ya ugonjwa wa saratani.

Utafiti huo, uliochapishwa jana na jarida la Nature, umebaini kuwa kujidhibiti kula tindikali ambatani (amino acid) ambayo hupatikana kwenye vyakula kama nyama nyekundu na mayai, kulisaidia matibabu ya saratani katika panya na kupunguza kasi ya kukua kwa uvimbe.

“Haya ni matokeo makubwa (ya udhibiti wa vyakula hivyo), na ni matokeo mazuri kama ambavyo tunavyoona dawa zikifanya kazi,” alisema kiongozi wa utafiti huo, Jason Locasale, ambaye ni profesa mshiriki wa Shule ya Uganga ya Chuo Kikuu cha Duke.

“Kitu ambacho utafiti huu unaonyesha ni kwamba kuna mazingira mengi ambayo dawa pekee haifanyi kazi, lakini kama ukichanganya dawa na chakula, inafanya kazi. Au tiba ya mionzi haifanyi kazi, lakini ukichanganya na chakula, inafanya kazi,” aliiambia AFP.

 

Utafiti huo ulijikita katika kudhibiti kula vyakula vyenye tindikali ambatani ya methionine (amino acid methionine) ambayo ni muhimu katika mchakato wa uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini (one-carbon metabolism) ambao husaidia seli za saratani kukua.

Pia Soma

Kuidhibiti Methionine, ambayo ni muhimu katika uvunjaji wa kemikali na afya ya seli nyingi, kumekuwa kukihusishwa na kudhibiti uzee na kupungua uzito, lakini umuhimu wake katika seli zenye saratani kunamaanisha kuwa kunaweza kuwa njia nzuri ya kuimarisha matibabu ya saratani.

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Agosti 2, 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz