Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuahirisha mambo, kutoyafanya kwa wakati chanzo cha msongo wa mawazo

74179 Mawazo+pic

Wed, 4 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Baadhi ya watu wana tabia ya kuanza jambo fulani walilopanga kufanya lakini kabla ya kufika mwisho wanaahirisha.

Kumbuka tabia yako ya kuahirisha mambo ni hatari kwa afya yako kwa sababu inaweza kukusababishia msongo wa mawazo ambao matokeo yake ni kupata shinikizo la damu na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza.

Unaweza kukuta mtu ameahirisha kufanya jambo muhimu kazini kwake lakini akaja kustuka wakati muda umeisha anatakiwa kuwa amekamilisha na hapo ndipo shinikizo la damu huanza.

Mtandao wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) umechapisha njia 10 za kukusaidia uache tabia ya kuahirisha mambo.

Baadhi ya njia hizo ni kutotegemea azma pekee kama motisha ya kukusaidia kufanya jambo kwa sababu kigezo hicho kinaweza kukufanya upuuzie sehemu muhimu ya kazi inayoweza kukufanya utimize malengo yako.

Pili, ni kutafakari manufaa ya kazi unayotaka kupuuzia. Watu wengi wameshindwa kufikia ndoto za maisha yao kwa sababu ya kupuuzia jambo bila kutafakari madhara au faida zake.

Pia Soma

Advertisement

Njia nyingine ni muhimu ili usiahirishe mambo ni kujiandaa mapema.

Wataalamu wa saikolojia wanasema, kujiandaa mapema kufanya jambo ni njia mojawapo ya kukufanya ushindwe kuahirisha kufanya kazi muhimu.

Jitahidi kuweka pembeni vitu vitakavyokushawishi kufanya jambo hilo mfano matumizi ya simu kupitiliza, kupiga soga na rafiki zako, ulevi au usingizi.

Lakini pia huwezi kumaliza mambo wakati muda wako mwingi unautumia kwenye mitandao ya kijamii. Jitahidi kupunguza tabia hiyo. Jipe nafasi ya kufanya kazi kwa bidii badala ya kupoteza muda mwingi huko.

Njia nyingine ni kujizawadia wewe mwenyewe. Utafiti uliofanywa na Catherine Milkman, kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, umegundua watu wakipewa nafasi ya kusikiliza hadithi ya kusisimua wakiwa kwenye ukumbi wa mazoezi pekee uwezekano wao kurudi kusikiliza kilichofanyika upo juu zaidi - Hadithi hiyo ni sehemu ya zawadi ya papo kwa papo.

Namna unavyojichukulia huathiri tabia yako. Wataalamu wanashauri kujenga tabia ya kujichukulia vizuri. Usijichukulie kama wewe ni mtu wa kushindwa ila mara zote ona jambo unalotaka kufanya lina mafanikio makubwa na utafanikiwa.

Mtaalamu wa masuala ya kisaikolojia kutoa Shirika la Msaada wa Kisaikolojia kwa Watoto (REPPSI) Edwick Mapalala anasema jambo muhimu ni kutengeneza orodha ya vitu unavyotaka kufanya, ukomo wa muda, jiambie nafanya sasa, fanya na jitahidi kuhakikisha kila siku inayopita uwe na jambo ulilofanya.

Chanzo: mwananchi.co.tz