Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kondomu milioni 60 kusambazwa

47220 Pic+condom

Tue, 19 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kufuatia uhaba wa mipira ya kiume maarufu kondomu uliojitokeza katika baadhi ya mikoa ikiwamo Njombe, Serikali inatarajia kusambaza kinga hizo milioni 60 ifikapo Juni.

Awali, Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ilisambaza kondomu milioni 31.6 kwa mwaka, lakini kutokana na kupokea jukumu la kuwa msambazaji mkuu wa bidhaa hiyo, idadi ya kondomu zitakazosambazwa kwa mwaka imeongezeka.

Akizungumza na Mwananchi juzi mkurugenzi mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu, alisema tayari kondomu zimesambazwa baadhi ya maeneo ikiwamo Njombe na kwamba licha ya kuongeza, watu hawaendi vituo vya afya kuomba kinga hizo.

“Kondomu zimekuwapo kwenye zahanati na vituo vya afya mkoani Njombe na wiki mbili zilizopita zilipelekwa 43,200, shida ilikuwa watu hawaji kuziomba,” alisema Bwanakunu.

Alisema kwa sasa katika maghala ya MSD kuna idadi ya kondomu milioni tisa, hivyo wamejipanga kuhakikisha zinafika maeneo yote ambayo awali hawakuyafikia.

Kabla ya kukabidhiwa jukumu la kununua na kusambaza, kondomu nchini zilisambazwa na baadhi ya wadau ikiwamo PSI.

Meneja miradi wa PSI, Alex Ngaiza, alipoulizwa kuhusu suala hilo na iwapo wao wameshindwa kusambaza kinga hizo kama awali, alisema: “Tulikuwa tunapewa fedha kutoka Global Fund... baada ya mradi kuisha walitangaza tenda na yakatokea mabadiliko.”



Chanzo: mwananchi.co.tz