Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kliniki ya macho Bugando kulaza wagonjwa 50

A464cdcf135980ebd522eaa9d9ccbb4c Mratibu wa mradi huo akifafanua uwezo wa kliniki

Tue, 5 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mradi wa Kuzuia Upofu Unaozulika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, unatarajiwa kuanza kazi rasmi Juni mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando mkoani Mwanza na ukikamilika kwa siku watakuwa wanalazwa wagonjwa 50.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mratibu wa mradi huo, Anthony Mhanda wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo na kusema kuwa kwa sasa hospitali hiyo inaweza kulaza wagonjwa 17 tu.

‘’Tunafanya mradi huu kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Christian Blind Mission (CBM),’’ amesema Mhanda.

Amesema kupitia mradi huo wa kliniki ya macho, utakuwa na uwezo wa kulaza kwa siku wagonjwa 50, tofauti na awali hospitali ya Bugando ilikuwa inalaza wagonjwa 17.

Amesema mradi huo ukianza kazi utahudumia wagonjwa wa mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, pamoja na mikoa ya Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma).

Amesema mradi huo ulianza kujengwa Machi 2021 na unatarajiwa kukamilika Aprili mwishoni mwaka huu.

Mhanda amesema hospitali yao ya Bugando, itakuwa inatumia madaktari bingwa mbalimbali kutoka hospitali hiyo, ili kuweza kuwatembelea wagonjwa wa macho waliopo majumbani, pamoja na kuwafikia wanafunzi wenye matatizo ya macho katika shule.

Naye Meneja Miradi kutoka CBM, Niwakheri Irira, amesema shirika lao litaendelea kushirikiana na hospitali ya Bugando kuweza kuwafikia wagonjwa wengi zaidi.

Alisema wamefanikiwa kujenga kliniki ya macho hospitali ya Ilembula mkoani Njombe pamoja na hospitali ya Kolandoto, Shinyanga.

Mkuu wa Idara ya macho hospital ya Bugando, Dk. Christopher Mwanansao, amesema kliniki hiyo ikikamilika itasaidia sana kupunguza msongamano wa wagonjwa waliokuwa wanatakiwa kusafiri kuelekea hospitali ya KCMC kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa macho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live