Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo kinachofuata kwa Chanjo jijini Mwanza

F25a35c91dfb4d46890c37c6a84a7225 Chanjo ya Uviko 19.

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: dailynews.co.tz

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa(RMO) amesema chanjo zinapatazo elfu 90 zimewasili jijini Mwanza.

Wakati wa uzinduzi wa chanjo hizo katika hospitali ya rufaa ya mkoa, Sekou Toure, Mganga mkuu Thomas Rutachunzibwa alisema kuna vituo 27 vya chanjo, kila Halamashauri ina vituo vitatu isipokuwa halamashauri ya jiji la mwanza ambalo linavituo vitano kutokana na idadi kubwa ya watu.

"Hii tumeifanya pia katika halamshauri ya sengerema ambapo tumeweka vituo vinne na kipaumbele ni makundi matatu kama ilivyotangazwa, watoa huduma za Afya, wale wenye umri wa miaka 50 na zaidi, pamoja na watu wanaosumbuliwa na magonjwa Sugu kama Kisukari, saratani na shinikizo la damu" alisema Mganga Mkuu.

Amedai kuwa, watu 1, 000 waliojiandikisha mtandaoni na ambao hawakujiandikisha walifika viwanjani hapo kwaajili ya kupata chanjo na kuwashauri waliochanja kuendelea kuchukua tahadhari zote za Uviko 19'Chanjo haizuii maambukizi lakini inamfanya mtu kuwa na nguvu ya kushinda ugonjwa huu ikiwa ataambukizwa" alisema.

Akizindua Hafla hiyo Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng Robert Gabriel ambaye alikuwa wa kwanza kupata chanjo hiyo, aliwatahadharisha wananchi kuwa 'wanaweza wakapata madhara baada ya chanjo ikiwa ni pamoja na ongezeko la joto mwilini saa chache baada ya kuchanjwa ambayo ni moja ya sifa za chanjo lakini haina Madhara". Pia amewashauri wananchi kuepuka taarifa za mitandaon zinazopotosha kuhusu chanjo.

Alisema, chanjo ya Corona ni sawa na Chanjo nyingine ambazo zimekuwa zikiingizwa kutoka nje ikiwa ni pamoja na ya Polio,"kwa sasa tuna ARVs kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi" dawa karibia zote zinatoka nje nchi na zinamanufaa kwa watumiaji wengi katika maeneo mbali mbali nchini. Alisema.

Chanzo: dailynews.co.tz