Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo cha Afya Yombo wapatiwa vifaa tiba vya kisasa

Yombo Kituo cha Afya Yombo wapatiwa vifaa tiba vya kisasa

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Afya Yombo Vituka Wilaya ya Temeke jijini Dar es saalam kimepata neema baada kupatiwa vifaa tiba vya kisasa kutoka kwa serikali.

Akiongea katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelwa amewaasa wahudumu katika Zahanati hiyo kuvitumia vifaa hivyo ipasavyo na kuvitunza.

“Vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa, ni wajibu wetu kuvitunza ili viweze kuhudumia maisha ya wanayombo na wengine kwa muda mrefu.” amesema Mabelwa

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Temeke Joketi Mwegelo amewahakikishia wananchi kupata huduma nzuri katika hospitali hiyo na kuwasihi kujiepusha na rushwa katika upatikanaji wa huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live