Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo cha Afya Sinza Palestina hakiwezi kuwa Hospitali ya Wilaya

9547 Sinza+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali imesema kuwa kituo cha afya cha Palestina kilichopo Kata ya Sinza jijini Dar es Salaam hakiwezi kuwa hospitali ya wilaya.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Juni 19 wakati Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege alipokuwa anajibu swali la mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema).

Katika swali la Kubenea ambalo liliulizwa na Joseph Selasini, ametaka kujua ni lini Serikali itaitambua hospitali hiyo kama hospitali ya wilaya kwa kuipa fedha na vitendea kazi vinavyofanana na hadhi yake kwa kuwa ni ahadi ya Rais.

Naibu Waziri amesema kwa mwaka wa fedha 2017/18, ruzuku ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliongezwa hadi kufikia Sh69milioni kutoka Sh57.40 milioni kwa mwaka wa fedha 2016/17.

“Kingine tumepeleka madaktari bingwa watatu kati ya watano wanaotakiwa, lakini pia kwa mwaka wa fedha 2018/19, kiasi cha Sh160 milioni kimetengwa kwa ajili ya kuendelea ujenzi wa jengo la ghorofa moja lenye wodi ya wanawake, wanaume na watoto,” amesema Kandege.

Kuhusu ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ubungo, amesema halmashauri ya wilaya ya Ubungo imeshaelekezwa kutenga eneo la ekari 25 litakalotumika kujenga majengo yote ya msingi ya hospitali ya wilaya.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz