Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kituo cha Afya Mnazi mmoja chapewa vifaa tiba, dawa

Ea5becaca77afae72bb49c1a26f83230 Kituo cha Afya Mnazi mmoja chapewa vifaa tiba, dawa

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imetoa Sh 261,833,200 kununulia ya vifaa tiba na dawa kwa ajili ya kituo cha afya cha Mnazi Mmoja katika manispaa ya Lindi.

Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Lindi, Abillahi Mbingu aliyasema hayo jana mjini hapa na kusema kuwa kati ya fedha hizo Sh milioni 86 ni kwa ajili ya ununuzi wa dawa na zilishapelekwa MSD na zilizosalia Sh 175,833,200 ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na vishaletwa na kufungwa katika kituo hicho.

Alisema kuwa vifaa hivyo vya tiba vitasaidia zaidi wagonjwa wale wenye shida ya upasuaji kama ngiri maji au kwenye uzazi, wakati uliopita huduma hiyo haikuwapo katika kituo hicho na kwa manispaa ya Lindi wagonjwa wao walikuwa wanategemea hospital ya Rufaa Sokoine, mkoani humo.

Kaimu Mganga huyo alisema kuwa wananchi wa kata za Mingoyo, Mnazimmoja na jirani watakuwa wakipata huduma za upasuaji katika kituo hicho ambacho pia kinatoa huduma baada ya kupatikana kwa wataalamu kama madaktari na wauguzi.

Aidha alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inawajali wananchi na ndio maana kituo hicho kimepatiwa wataalamu kama madaktari, wauguzi na wataalamu wa afya kutoka serikali kuu.

Aliishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuongeza vituo vya afya kama Kitoamanga, Mnazi Mmoja, Kineng'ene ambapo miaka ya nyuma kituo kilikuwa kimoja cha mjini Lindi.

Chanzo: habarileo.co.tz