Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kitimoto chatajwa kusababisha kifafa!

Kitimoto Kitimoto chatajwa kusababisha kifafa!

Tue, 15 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari Bingwa wa mishipa ya fahamu na utindio wa Ubongo Dr. Yusuf Jamnagerwalla amesema ulaji wa nyama ya nguruwe maarufu ‘kitimoto’ husababisha kifafa iwapo hakijapikwa vizuri.

"Ugonjwa wa kifafa unatibika, ukimwona Mtu ana dalili za kifafa asifikirie kwamba amelogwa au ana mashetani/mapepo hapo ndio kila kitu kinaharibika, ukiona dalili hizo nenda kituo cha afya na kuwaachia Wataalamu wafanye kazi yao na mgonjwa atapatiwa matibabu na madawa yapo"

"Kila Jumatatu ya pili ya Februari ni siku ya kifafa na kuna Watu zaidi ya milioni 95 wanaishi na ugonjwa wa kifafa ambapo kato yao 60% hadi 70% wako kwenye nchi masikini na Nchi zinazoendelea, changamoto kubwa ni upatikanaji wa dawa"

"Kuna uhusiano kati ya ugonjwa wa akili na kifafa lakini sio wote wenye ugonjwa wa akili wana kifafa ila dalili za ugonjwa wa akili zinafanana na za ugonjwa wa kifafa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live