Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisukari, shinikizo la damu vyachangia upofu

Kisukari 640x400 Kisukari, shinikizo la damu vyachangia upofu

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAGONJWA yasiyo ya kuambukiza ikiwamo kisukari na shinikizo la juu la damu yametajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ugonjwa wa macho nchini.

Haya yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma za tiba Wizara ya Afya, Dk Mwinyiko Amiri kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho Duniani kilichofanyika kitaifa jijini hapa.

Alisema tafiti zilizopita pamoja na taarifa mbalimbali za afya zimeonesha kuwa kuna ongezeko la magonjwa ya macho hasa yanayosababishwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama kisukari na mengine.

Alisema tatizo la macho linalosababishwa na shinikizo la juu la damu limeongezeka kwa asilimia 31 kutoka wagonjwa 3,800 mwaka 2021 hadi 5,571 mwaka 2022.

Dk Mwinyiko alisema mwaka huu wanaendesha utafiti wa hali ya ulemavu wa kutokuona na upungufu wa kuona katika Mkoa wa Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live