Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kinondoni kinara matende, mabusha

Matende Kinondoni kinara matende, mabusha

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

AGONJWA yasiyopewa kipaumbele ya Mabusha na Matende, bado yanaendelea kusumbua kata 10 za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, kutokana na kuwepo kwa maambukizi mapya.

Hayo yamebanishwa leo tarehe 12 Machi 2024, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akielezea tathimini iliyofanywa na Serikali kuhusu magonjwa hayo kati ya Agosti 2023 na Februari 2024.

Ummy ametaja kata hizo kuwa ni, Tandale, Kijitonyama, Mwananyamala, Kigogo, Mzimuni, Magomeni, Ndugumbi, Hananasif, Kinondoni na Makumbusho.

“Katika Jiji la Dar es Salaam hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa matende na mabusha, isipokuwa tumebakiwa na Manispaa ya Kinondoni. Tathimini tumefanya Kinondoni katika kata 10 hazina maambukizi mapya lakini tumebakiwa na kata 10 na tathimini imeonesha bado zina maambukizi mapya kwa kiwango cha asilimia 2.5,” amesema Ummy.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, itaendesha zoezi la utoaji kinga tiba kwa wananchi wa kata hizo, ndani ya muda wa miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live