Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kikosi kazi kupambana na mbu waenezao Dengue chaanzishwa

63393 Pic+dengue

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali ya Tanzania imeanzisha kikosi kazi cha wataalam kwa ajili ya kuangamiza mbu wanaoeneza ugonjwa wa dengue.

Amesema watalaam hao pamoja na mambo mengine watashauri kama dawa zinazotumika sasa kuangamiza mbu hao zinafaa ama la.

Ummy ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu.

Katika swali lake Zungu amesema ugonjwa wa dengue katika Mkoa wa Dar es Salaam bado ni changamoto na kuhoji kama Serikali ipo tayari kubadili dawa, kwa kuwapatia wananchi dawa za chenga ili kuzimwaga katika maeneo mbalimbali kutokomeza mazalia ya mbu hao.

“Tayari suala hili linafanyiwa kazi katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na siku mbili zijazo Serikali itatoa tamko bungeni kuhusu taratibu mbalimbali za kupambana na dengue.”

“Pia, tumeanzisha kikosi cha wataalam wa kuangamiza mbu ili pamoja na mambo mengine watueleze kama dawa tunazotumia zinafaa au hazifai,” amesema Ummy.

Pia Soma

Ukweli kuhusu dengue

Ni ugonjwa unaoenezwa na mbu aina ya Aedes, mbu mweusi mwenye madoa doa meupe ya kung’aa ambaye hupendelea kuuma hasa wakati wa asubuhi, mchana na jioni.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na homa ya ghafla, kuumwa na kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati siku ya tatu hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya dengue.

Aidha, mgonjwa wa homa ya dengue mara chache hupata vipele vidogovidogo, anavilia damu kwenye ngozi na wengine kutokwa na damu sehemu za fizi, mdomoni, puani, kwenye macho na pia kwenye njia ya haja kubwa au ndogo.

Chanzo: mwananchi.co.tz