Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kijana 'shoga' asimulia A-Z alivyoambukizwa UKIMWI "Nimeokoka"

Kimanti Vvu Kijana 'shoga' asimulia A-Z alivyoambukizwa UKIMWI "Nimeokoka"

Fri, 22 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Duncan Kimathi, raia wa Kenya anayeishi na virusi vya UKIMWI, amewatia moyo wenzake wanaoishi na virusi hivyo huku akiwataka kutokata tamaa maishani.

Katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini humo kuhusu masuala ya mahusiano, Kimathi alisimulia namna alipata virusi hivyo vya Ukimwi na jinsi maisha yake yalibadilika.

“Marafiki zangu walinitambulisha kwa ushoga mwaka wa 2015 baada ya kumaliza shule ya sekondari mwaka wa 2014. Maisha yalikuwa magumu, na nilikuwa nikihangaika, nikajikuta nimeingia kwenye vitendo hivyo,” alisema.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 28, alisema siku moja mwaka 2016, aliugua na baada ya kuenda hospitalini alifanyiwa vipimo kadhaa na kugundua kuwa ana virusi vya Ukimwi.

"Siku za kwanza alikuwa anatumia PEP lakini baada ya kupima, hatumii dawa tena, tunapanga kupata mtoto hivi karibuni," alisema. Mwanamume huyo shupavu alisema mke wake ndiye aliyemchochea kuacha ushoga, akisema alivutiwa naye kwa sababu alikuwa na moyo mwema.

Kimathi alisema: "Unapojihusisha na ushoga, hauthamini wanawake, hauwaoni kama watu muhimu maishani." Alimumiminia mke wake sifa akisema ni mkombozi wake.

"Ni mkombozi wangu. Alinisaidia nitoke mahali mbaya (Alinisaidia kuacha tabia yangu mbaya). Sijui ningekuwa wapi sasa bila yeye."

Jamaa huyo mpole alisema hajawahi kuwafichulia wazazi wake kuhusu hali yake na ni mkewe na rafiki yake mmoja tu ndio wanajua. Kimathi ambaye kwa sasa ameokoka aliwashauri wanaoishi maisha kama yake ya zamani kumkubali Yesu.

"Ukijua ulipata Ukimwi kupitia nini (ukijua jinsi ulivyoambukizwa HIV), acha unachofanya na uanze maisha mapya, watu wanajiunga na ushoga kwa ajili ya starehe...okoka na maisha yako yatabadilika na kuwa bora. Ukimwi sio hukumu ya kifo," alishauri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live