Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigwangalla: Nipo salama, nawashukuru Watanzania

10250 KIGWANGALLA2+PIC TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla ametolewa katika wodi ya Mwaisela na kupelekwa katika chumba cha maabara kwa ajili ya kufanyiwa X-Ray ya kifua.

Akizungumza na MCL Digital leo mchana Agosti 5, 2018 kabla ya kupelekwa katika vipimo zaidi, Dk Kigwangalla amewashukuru madaktari kwa huduma walizompatia, wakiwemo wa mkoani Manyara na Arusha.

Pia, amemshukuru Rais John Magufuli, katibu wa Bunge, Dk Stephen Kagaigai na viongozi wa Serikali kwa ushirikiano waliompa.

Mdogo wa wa waziri huyo, Halima Mrisho amesema kaka yake anaendelea vyema na matibabu. Amewashukuru wote waliomsaidia.

Dk Kigwangalla alipata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini. Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba alifariki dunia.

Awali, Kigwangalla alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helikopta na kisha kuletwa Muhimbili jana jioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz