Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigwangala kuendelea na matibabu akiwa nyumbani

16928 Pic+kigwa TanzaniaWeb

Wed, 12 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.Waziri wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangala aliruhusiwa jana kutoka hospitali na sasa anahudumiwa akiwa nyumbani.

Dk Kigwangala alikuwa amelazwa katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI) baada kupata ajali Julai mwaka huu  akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Manyara. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga ameliambia bunge leo Septemba 12, 2018 kuwa Kigwangala aliruhusiwa jana na sasa yupo nyuMbani kwake.

Hasunga amewashukuru wabunge na Watanzania kwa kumuombea kiongozi huyo akisema kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika.

Chanzo: mwananchi.co.tz