Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kigoma yapunguza vifo vya wajawazito, watoto wachanga

Kupandikiza Mimba (600 X 468) Kigoma yapunguza vifo vya wajawazito, watoto wachanga

Fri, 28 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoa wa Kigoma umefanikiwa kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga kutoka vifo vitokanavyo na uzazi 119 kwa mwaka 2020 hadi 75 kwa mwaka 2021 na vifo vya watoto wachanga kutoka 1147 kwa mwaka 2020 hadi 990 kwa mwaka 2021.

Hatua hiyo imekuja tangu mkoa huo kuzindua mpango wa dharura wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2021, vilivyokuwa vimeongezeka kwa asilimia 95 katika vituo vya afya.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Januari 28, 2022 Mratibu wa huduma ya afya ya uzazi na mtoto, Bernadetha Peter amesema mpango huo umeweza kuwasaidia kwa kutekeleza shuguli mbalimbali ikiwemo kutoa mafunzo ya huduma muhimu kwa watoto wachanga.

Amesema wanafanya usimamizi shirikishi katika vile vituo ambavyo vinatoa huduma muhimu kwa kina mama wajawazito, wanafanya ushirikishwaji wa kesi yoyote ambayo ni ngumu asikae nayo anatoa taarifa katika makundi ya whatsap ambayo yametengenezwa maalumu ili kuweza kusaidiwa kwa haraka kwani njia hiyo imesaidia sana.

Amesema pia mkoa umetengeneza timu ya kutathmini vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga katika ngazi ya mkoa ambapo ikitokea kifo katika wilaya timu hiyo inakwenda kujadili nao kwa pamoja  kwa kushirikiana na timu ya wilaya ili kujua changamoto zipi zimetokea hadi kupelekea kifo  na kuweka mpango mkakati  wa pamoja na kufanya utekelezaji.

Bernadetha amesema kuna vituo maalum ambavyo vinatoa huduma maalum kwa kina mama wajawazito ambapo vinafanya upasuaji na kuongezea damu na huduma za kuzalisha hapo pia timu ya wataamu ya mkoa wanapita kwenye vituo hivyo na kuwajengea uwezo watoa huduma lengo ni kuboresha huduma.

“Manispaa ya kigoma ujiji ndio inaongoza kwa idadai kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga, ikifatiwa na wilaya ya Kasulu na Uvinza kutokana na jografia ya wilaya hiyo ilivyokaa ni sababu ya kupelekea vifo,”amesema Bernadetha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live