Dar es Salaam. Licha ya Serikali kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwenda kwenye vituo vya afya na hospitali kupimwa pindi wanapoona dalili za kifua kikuu (TB), kuna baadhi huenda kwa waganga wa kienyeji kupata tiba.
Msanii wa ngoma za asili kutoka kikundi cha Mukikute jijini Dar es Salaam, Gota Ngogota ni miongoni mwa waliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji kupata tiba, akidhani amerogwa kabla hajagundua kama anaumwa TB.
Takwimu za Serikali zinaonyesha watu watatu hufariki dunia kila baada ya saa moja nchini kwa sababu ya TB sawa na idadi ya watu 70 kila siku.
Akizungumza kwenye mkutano wa kwanza wa ushiriki wa wadau katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo unaojulikana kwa jina la ‘Stop TB Partnership’ ulioandaliwa na Health Promotion Tanzania wakishirikiana na Serikali hivi karibuni, Ngogota alisema aliamini amerogwa kwa sababu homa zilizokuwa zinamkumba hakujua zinasababishwa na nini.
“Zilianza dalili za kawaida tu, nikajua ugonjwa wa kawaida lakini baadaye nilishangaa napata joto kali, nakohoa mfululizo na usiku natoka jasho jingi sana nikajua nitakuwa nimerogwa siyo bure,” anasema Ngogota.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kifua kikuu ndiyo ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza duniani.
Pia Soma
- Lukuvi awaita Dodoma wadaiwa kodi za pango, ni mashirika na taasisi 270
- Mawaziri wa Nishati EAC kukutana Arusha, timu za maandalizi zaanza kuteta
- Imarisha maelewano na wafanyakazi wenzako kwa njia hii
- Rais Museveni ‘amu-unfollow’ Jose Chameleone kwenye twitter baada ya kujiunga na siasa
Kwa simulizi zaidi ya msanii huyo, soma Jarida la Afya kesho Ijumaa Juni 7, 2019 katika gazeti la Mwananchi.